WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA KIISLAMU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE WAKARIBISHWA CHUONI HAPO, YAFANYWA HARAMBE, SH. MILIONI 12 ZAPATIKANA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau, akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Kiislam na harambe ya kuchangia mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislam wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni Dar es Salaam leo, ambapo katika harambe hiyo, sh. milioni 12 zilipatikana kwa ajili ya kutunisha mfuko wa Jumuiya. Katikati ni Mhadhiri wa Dini ya Kiislam, Sheikh Ramadhan Mbukuzi na Amiri wa wanafunzi wa Kiislamu chuoni hapo, Mhini Mganga. (Picha zote na Kassim Mbarouk) Baadhi ya wanafunzi wa Kiislam wa Mwaka wa kwanza, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau, awakati alipokuwa kizungumza katika hafla ya kuwakaribisha pamoja na harambe ya kuchangia mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislam wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni Dar es Salaam leo, ambapo katika harambe hiyo, sh. milioni 12, zilipatikana...