PROFESA MWAKALILA AWAASA WANAFUNZI MWALIMU NYERERE KUACHANA NA SIASA WAKIWA SHULENI
Na Mwandishi wetu , MNMA MKUU wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo kigamboni,Profesa , Shadrack Mwakalila ameagiza wanafunzi wa chuo hicho, waliojiunga katika mwaka wa Masomo wa 2017 kutojiusisha na masuala ya siasa pindi wanapokuwa chuo na badala yake wazingatie katika suala zima la taaluma ili waweze kupata kile kilicho wapeleka chuoni hapo. Profesa Mwakalila amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Mwaka wa kwanza juu ya nini wanatakiwa kufanya wakiwa chuoni hapo na kutambua nini cha msingi kilichowaleta. "Hapa sio mahali pakufanya Siasa ni sehemu mliyokuja kuchukua taaluma, kamwe msikubali wanasiasa kuwatumia kwa ajili ya maslahi yao kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmepoteza lengo ambalo limewaleta hapa katika kufanikisha malengo yenu ya kitaaluma"amesema Profesa Mwakalila. Profesa Mwakalila ameongeza kuwa kama wanavyojua chuo hicho kimetokana na Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius .K. Nyerere hivyo wa...