PROFESA MWAKALILA AWAASA WANAFUNZI MWALIMU NYERERE KUACHANA NA SIASA WAKIWA SHULENI
Na Mwandishi wetu , MNMA
MKUU wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo kigamboni,Profesa , Shadrack Mwakalila ameagiza wanafunzi wa chuo hicho, waliojiunga katika mwaka wa Masomo wa 2017 kutojiusisha na masuala ya siasa pindi wanapokuwa chuo na badala yake wazingatie katika suala zima la taaluma ili waweze kupata kile kilicho wapeleka chuoni hapo.
Profesa Mwakalila amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Mwaka wa kwanza juu ya nini wanatakiwa kufanya wakiwa chuoni hapo na kutambua nini cha msingi kilichowaleta.
"Hapa sio mahali pakufanya Siasa ni sehemu mliyokuja kuchukua taaluma, kamwe msikubali wanasiasa kuwatumia kwa ajili ya maslahi yao kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmepoteza lengo ambalo limewaleta hapa katika kufanikisha malengo yenu ya kitaaluma"amesema Profesa Mwakalila.
Profesa Mwakalila ameongeza kuwa kama wanavyojua chuo hicho kimetokana na Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius .K. Nyerere hivyo wanapaswa kufuata maadili na kuwa waadilifu ili kumuenzi muasisi Baba wa Taifa ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa sehemu hiyo iweze kupika viongozi wenye maadili mema kwa Taifa hili.
alimaliza kwa kutoa wito kwa wote waweze kukazana katika masomo yao hili waweze kuwa alama ya chuo hicho pindi wanapomaliza masomo yao na kufika hapo kwao isiwe majuto.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam,Profesa. Shadrack Mwakalila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo hicho wa Mwaka wa kwanza ambao wamechaguliwa katika muhula wa Masomo 2017 kwa ngazi ya Cheti, Astashahada na Shahada juu ya umuhimu wa kufuata Maadili.
Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akikazia jambo juu ya kuwa na maadili shuleni
Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila
Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila
Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila
Comments
Post a Comment