DKT SHEIN AFUNGUA KONGAMANO LA KWANZA LA HAYATI SHEIKH ABEID AMANI KARUME KAMPASI YA BUBU
Na Mwandishiwetu, Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amewaasa vijana wa Zanzibar kuwa Wazalendo na nchi yao kwa kuisoma na kuijua historia ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuenzi mchango wa Mwasisi wa Taifa hilo Hayati Sheikh Abeid Amani Karume. Dkt. Shein ameyasema hayo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika kongamano la kwanza la kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, lililofanyika katika Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika kampasi ya Zanzibar, iliyopo Bububu mjini Magharibi siku ya Alhamis tarehe 5 April, 2018. “Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa ni mtu mvumilivu na mstahimilivu, aliyeipenda Zanzibar na wananchi wake, hivyo ni vyema mchango wake katika kuleta maendeleo ya Zanzibar ukakumbukwa na kuenziwa. Rais Karume ametumia fursa hiyo pia kukiponge...