DKT SHEIN AFUNGUA KONGAMANO LA KWANZA LA HAYATI SHEIKH ABEID AMANI KARUME KAMPASI YA BUBU
Na Mwandishiwetu, Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amewaasa vijana wa Zanzibar kuwa Wazalendo na
nchi yao kwa kuisoma na kuijua historia
ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuenzi mchango wa Mwasisi wa Taifa hilo Hayati
Sheikh Abeid Amani Karume.
Dkt.
Shein ameyasema hayo wakati akitoa
hotuba ya ufunguzi katika kongamano la
kwanza la kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa kwanza wa
Baraza la mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, lililofanyika katika Chuo cha kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere katika kampasi ya
Zanzibar, iliyopo Bububu mjini Magharibi
siku ya Alhamis tarehe 5 April, 2018.
“Hayati
Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa ni mtu mvumilivu na mstahimilivu,
aliyeipenda Zanzibar na wananchi wake, hivyo ni vyema mchango wake katika
kuleta maendeleo ya Zanzibar ukakumbukwa na kuenziwa.
Rais Karume ametumia fursa hiyo pia
kukipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuona umuhimu wa kuandaa
Kongamano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika visiwani Zanzibar”
“Chuo
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imeandaa Kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya
kuwaenzi waasisi wa Taifa ambao ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati
Abeid Amani Karume ambao wanamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa” amesema
Rais Shein.
Katika
taarifa yake, Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof.Shadrack Mwakalilia alieleza kuwa Hayati sheikh Abeid Amani
Karume alipigania mengi kwaajili ya ustawi wa Zanzibar, na ndio sababu Chuo kikaona umuhimu wa kuandaa
kongamano hilo kwa lengo la kujikumbusha
na kujadili falsafa na ndoto za Sheikh Abeid Amani Karume katika ustawi wa
Zanzibar ya leo.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Prof.Mark
Mwandosya alimuahidi Dkt. Shein kuwa Chuo
kitaendeleza utamaduni wa kufanya makongamano kila mwaka kwa lengo la kumuenzi muasisi wa Zanzibar na
pia kuwakumbusha vijana historia
ya Zanzibar ya sasa kupitia mchango mkubwa uliotolewa na Mwasisi wa Zanzibar
Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Mwenyekiti
wa Kongamano hilo alikuwa Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.
Pandu Ameir Kificho ambapo watoa mada walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda
Balozi Amina Said Ali ambae alitoa mada kuhusu “Fikra za Abeid Amani Karume na
mapinduzi ya Uchumi Zanzibar” na Mhe. Mohamed Seif Khatib ambae alitoa mada
kuhusu “Fikra za Abeid Amani Karume katika kujenga umoja na mshikamano wa
kijamii Zanzibar.
Wadau mbali mbali wakiwemo baadhi ya viongozi
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walishiriki na kuchangia katika mada hizo.
Katika
hatua nyingine, Rais Dkt. Shein aliwatunuku vyeti na zawadi wanafunzi wa skuli
za msingi na sekondari Zanzibar ambao walifanya vizuri katika shindano la
uandishi wa insha kuhusu mchango wa Sheikh Abeid Amani Karume katika maendeleo
ya Zanzibar.
Hayati
Sheikh Abeid Amani Karume alifariki
April 7, 1972.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya
ufunguzi wakati wa kongamono la kumbukumbu ya hayati sheikh abeid amani karume
lililoandaliwa na chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere kampasi ya zanzibar.
1. Mgeni rasmi katika
kongamano Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya
pamoja na meza kuu pamoja na Wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari
waliofanya vizuri katika uandishi wa insha juu ya mchango wa Sheikh Abeid Amani Karume katika maendeleo ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment