CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KUFANYA MASOMO YA UZALENDO NA MAADILI KUWA NI LAZIMA KWA KILA KOZI
Na Mwandishi wetu MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema Chuo chake kitaanza kutoa Somo la Uzalendo,Uadilifu na Maadili kuwa ni lazima katika kila kozi itakayotolewa na Chuo hicho. Profesa Mwakalila amesema hayo leo alipokuwa akifungua Mhadhara wa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana uliofanyika katika ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere. “Tutapitia mitaala yote hili kuweza kuongeza masuala ya maadili na Uongozi hivyo kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 Chuo chetu kitaanza kutoa Masomo ya Uongozi, Maadili na Uzalendo kama Masomo ya lazima katika kila kozi itakayotolewa chuoni hapa mitaala yote ipo katika hatua za mwisho na imefikishwa katika mamlaka zinazohusika hili ziweze kurejeshwa shuleni” Profesa Mwakalila amesema kuwa utaratibu wa kutoa mada mbalimbali kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuhusu uongozi, Maadili na utaifa umeshaandaliwa . Kwa upande wake mmoja wa watoa mada katika Mhadhara huo Ibrahim K...