CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KUFANYA MASOMO YA UZALENDO NA MAADILI KUWA NI LAZIMA KWA KILA KOZI

Na Mwandishi wetu

MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema Chuo chake kitaanza kutoa Somo la Uzalendo,Uadilifu na Maadili kuwa ni lazima katika kila kozi itakayotolewa na Chuo hicho.

Profesa Mwakalila amesema hayo leo alipokuwa akifungua Mhadhara wa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana uliofanyika katika ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere.

“Tutapitia mitaala yote hili kuweza kuongeza masuala ya maadili na Uongozi hivyo kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 Chuo chetu kitaanza kutoa Masomo ya Uongozi, Maadili na Uzalendo kama Masomo ya lazima katika kila kozi itakayotolewa chuoni hapa mitaala yote ipo katika hatua za mwisho na imefikishwa katika mamlaka zinazohusika hili ziweze kurejeshwa shuleni”

Profesa Mwakalila amesema kuwa utaratibu wa kutoa mada mbalimbali kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuhusu uongozi, Maadili na utaifa umeshaandaliwa .
Kwa upande wake mmoja wa watoa mada katika Mhadhara huo  Ibrahim Kaduma aliwakumbusha Vijana hao juu ya umuhimu wa kuwa Wazalendo kwa kuwasomea ahadi za Tanu kuwa kama Muongozo wa kutunza maadili katika kazi zao za kila siku.

Kaduma pia alitumia mahadahara huo kuwaambia Vijana juu ya umuhimu wa azimio la Arusha katika kujiletea misingi la Maendeleo hivyo kumuagiza kila kijana wa chuo hicho kwenda kusoma azimio hilo kwa umakini.

Kwa upande mtoa Mada Mwingine Samuel Kassori alizungumza juu ya uadilfu na kusema ni vyema viongozi wakalejea kusoma baadhi ya hotuba za Mwalimu na kusisitiza juu ya hotuba ile ya jisahiishe ambayo imezungumza namna ya Mwalimu Nyerere alivyoandika juu ya umuhimu kwa kila mmoja kujitathmini katika kazi za Serikali.

Amesema Viongozi wengi wameshindwa kumsaidia Rais John Magufuli matokeo yake wamekuwa wakifanya kazi kwa kukurupika bila ya kuwafikilia watanzania waliopo nyuma yao.
 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo hicho wakati wa Mhadhara wa wa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana kama njia ya kuenzi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
Samuel Kassori  Mtoa Mada katika Mhadharawa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana kama njia ya kuenzi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere  
 Ibrahim KadumaMtoa Mada katika Mhadharawa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana kama njia ya kuenzi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere  
 Afisa Habari wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Evelyn Mpasha akizungumza jambo na Wanafunzi wa Chuo Hicho.
Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakifatilia Mhadhara wa wa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana kama njia ya kuenzi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Comments

Popular posts from this blog

DKT SHEIN AFUNGUA KONGAMANO LA KWANZA LA HAYATI SHEIKH ABEID AMANI KARUME KAMPASI YA BUBU

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHAFANYA KONGAMANO KUHUSU UADILIFU NA UTAWALA BORA KATIKA KUSIMAMIA RASILIMALI ZETU

WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA KIISLAMU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE WAKARIBISHWA CHUONI HAPO, YAFANYWA HARAMBE, SH. MILIONI 12 ZAPATIKANA