Posts

DKT SHEIN AFUNGUA KONGAMANO LA KWANZA LA HAYATI SHEIKH ABEID AMANI KARUME KAMPASI YA BUBU

Image
Na Mwandishiwetu, Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein  amewaasa vijana wa Zanzibar kuwa Wazalendo na nchi yao  kwa kuisoma na kuijua historia ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuenzi mchango wa Mwasisi wa Taifa hilo Hayati Sheikh Abeid Amani Karume. Dkt. Shein  ameyasema hayo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika  kongamano la kwanza la kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume,  lililofanyika katika Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere   katika kampasi ya Zanzibar, iliyopo Bububu  mjini Magharibi siku ya Alhamis tarehe 5 April, 2018. “Hayati Sheikh Abeid Amani Karume,   alikuwa ni mtu mvumilivu na mstahimilivu, aliyeipenda Zanzibar na wananchi wake, hivyo ni vyema mchango wake katika kuleta maendeleo ya Zanzibar ukakumbukwa na kuenziwa. Rais Karume ametumia fursa hiyo pia kukiponge...

KIMEI ATOA SOMO MNMA

Image

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KUFANYA MASOMO YA UZALENDO NA MAADILI KUWA NI LAZIMA KWA KILA KOZI

Image
Na Mwandishi wetu MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema Chuo chake kitaanza kutoa Somo la Uzalendo,Uadilifu na Maadili kuwa ni lazima katika kila kozi itakayotolewa na Chuo hicho. Profesa Mwakalila amesema hayo leo alipokuwa akifungua Mhadhara wa Uzalendo , Utaifa na Uadilifu kwa Vijana uliofanyika katika ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere. “Tutapitia mitaala yote hili kuweza kuongeza masuala ya maadili na Uongozi hivyo kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 Chuo chetu kitaanza kutoa Masomo ya Uongozi, Maadili na Uzalendo kama Masomo ya lazima katika kila kozi itakayotolewa chuoni hapa mitaala yote ipo katika hatua za mwisho na imefikishwa katika mamlaka zinazohusika hili ziweze kurejeshwa shuleni” Profesa Mwakalila amesema kuwa utaratibu wa kutoa mada mbalimbali kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuhusu uongozi, Maadili na utaifa umeshaandaliwa . Kwa upande wake mmoja wa watoa mada katika Mhadhara huo  Ibrahim K...

MAKTABA YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YAWA KITOVU CHA MAARIFA

Image
 Mmoja wa Wanafunzi wa chuo  cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa katika maktaba ya chuo hicho iliyosheeni vitabu  katika nyanja mbalimbali, akichagua moja ya vitabu aweze kuongeza maarifa  Baadhi ya Wanafunzi wakichagua vitabu kwa ajili ya kujisomea  ndani ya maktaba ya chuo  wanafunzi wakijisomea katika Maktaba ya Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere  Wanafunzi wakijisomea Magazeti ndani ya Maktaba ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA ASEMA UWEPO WA VIWANDA UTAKUZA KILIMO NCHINI

Image
Na Mwandishi wetu NAIBU Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema uwepo wa viwanda nchini utachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa bidhaa za kilimo kwa kuwahakikishia wakulima wanakuwa na soko la uhakika. Mhandisi Manyanya ameyasema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa k ongamano la wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza viwanda nchini lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA). Amesema ili  kufikia malengo hayo kunahitajika ushirikiano mkubwa kati ya sekta binafsi na Serikali  kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara. "Tasisi za fedha mnatakiwa kuhakikisha mnatatua changamoto za wajasiriamali za ukosaji wa mitaji jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wengi wao, ili kuhakikisha tunafikia Tanzania ya viwanda" amesema. Mhandisi Manyama, amesisitiza ikiwa taasisi za fedha zitasaidia kukuza uchumi kupitia viwanda maana yake itakuwa chachu ya kukuza kipato cha wawekezaji na kuongeza mnyororo wa t...

PROFESA MWAKALILA AWAASA WANAFUNZI MWALIMU NYERERE KUACHANA NA SIASA WAKIWA SHULENI

Image
Na Mwandishi wetu , MNMA  MKUU wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo kigamboni,Profesa , Shadrack Mwakalila    ameagiza wanafunzi wa chuo hicho, waliojiunga katika mwaka wa Masomo wa 2017 kutojiusisha na masuala ya siasa pindi wanapokuwa chuo na badala yake wazingatie katika suala zima la taaluma ili waweze kupata kile kilicho wapeleka chuoni hapo. Profesa Mwakalila amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Mwaka wa kwanza juu ya nini wanatakiwa kufanya wakiwa chuoni hapo na kutambua nini cha msingi kilichowaleta. "Hapa sio mahali pakufanya Siasa ni sehemu mliyokuja kuchukua taaluma, kamwe msikubali wanasiasa kuwatumia kwa ajili ya maslahi yao kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmepoteza lengo ambalo limewaleta hapa katika kufanikisha malengo yenu ya kitaaluma"amesema Profesa Mwakalila. Profesa Mwakalila ameongeza kuwa kama wanavyojua chuo hicho kimetokana na Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius .K. Nyerere hivyo wa...

WATANZANIA WATAKIWA KUMUENZI MWALIMU NYERERE KWA KUTUMIA MAPINDUZI YA VIWANDA

Image
Na  Mwandishi wetu, MNMA                                                                                                                                                                                                                                                                                    ...